As-salamu alaykum Mhe. Rais Samia. Pole kwa Majukumu. Wewe ndiye Rais wetu na hatuna mwingine. Umesema kila mtu ana haki juu ya Tanzania, na hakuna aliye juu ya sheria. Rais Samia, Watanzania ni watu wema, ukiwa Kiongozi wao, wanataka kujua kuhusu Bandari. Wanataka kujua kwa nini Polisi wanawazuia Wapinzani hasa CHADEMA kwenda kufanya mikutano Ngorongoro…