Nairobi, Kenya
Kampuni ya SpaceX inayotoa huduma za internet kupitia Starlink imetangaza leo Julai 18, 2023 kuanza kutoa huduma zake nchini Kenya.
Starlink ni mradi wa setilaiti za mtandao ulioanzishwa na kampuni ya anga ya juu ya SpaceX, iliyoanzishwa na Elon Musk. lengo kuu la Starlink ni kutoa ufikiaji wa intaneti wa kasi na wa chini wa kuchelewa kwa maeneo yaliyo na huduma duni ya intaneti au yaliyo mbali na maeneo ya maendeleo duniani kote. Mradi huu unalenga kubadilisha ufikiaji wa intaneti, haswa katika maeneo ya vijijini na yale ambayo miundombinu ya intaneti ya kawaida ni chache au haipo kabisa.
TANZANIA JE, LINI HUDUMA ITAFIKA?
Tarehe 5 Februari, 2023 Mmiliki wa Kampuni ya SpaceX inayotoa huduma ya internet kupitia Starlink Elon Musk aliombwa kuleta huduma Tanzania, kama inavyoonekana katika tweet

Elon Musk katika kujibu tweet hiyo alikiri kupeleka taarifa za maombi ya kutambulisha huduma ya internet ya Starlink Tanzania ambapo alisema kuwa ameshawasilisha nyaraka muda mrefu katika Serikali ya Tanzania na anasubiri uidhinishaji wa nyaraka hizo.
Setilaiti za Mtandao: Starlink inalenga kuzindua setilaiti nyingi ndogo katika anga ya chini ya Dunia (LEO). Setilaiti hizi hufanya kazi pamoja ili kuunda mtandao ambao unaweza kutoa huduma za intaneti kwenye uso wa Dunia. Kufikia mwaka 2021 SpaceX ilikuwa tayari imezindua setilaiti nyingi za Starlink, na walikuwa na mipango ya kupeleka maelfu mengine katika miaka ijayo.
Watanzania wengi walionekana kuunga moono suala hilo akiwemo mfanyabiashara Mohammed Dewji alipo comment na kusema atasaidia kushughulikia kwa Serikali ili kufanikisha huduma hiyo ya internet ya Starlink inapatikana Tanzania, Mo Dewji aliandika

Anga ya Chini ya Dunia: Tofauti na setilaiti za kawaida za geostationary ambazo zinazunguka mbali zaidi na Dunia, setilaiti za Starlink zinafanya kazi katika anga ya chini ya Dunia, kawaida kwenye umbali kati ya kilomita 340 hadi 1,200 juu ya uso wa Dunia. Umbali huu wa chini husababisha kuchelewa kidogo na kasi kubwa ya uhamisho wa data ikilinganishwa na huduma za intaneti za setilaiti za kawaida.
MJADALA MKALI, WAZIRI WA HABARI NAPE NNAUYE AZUNGUMZA.
Baada ya mjadala kuwa mrefu ulioonesha ukwamaji wa uidhinishwaji wa nyaraka kutoka Serikalini kumruhusu Elon Musk kupitia Starlink kuwezesha huduma za internet Tanzania na wananchi kumtaka Waziri wa Habari Nape Nnauye atoe maelezo, Waziri alitoka na kujibu kuwa walipokea nyaraka za maombi za Starlink kutoa huduma Tanzania lakini hawakupitisha kwa kuwa Starlink hawakutimiza vigezo na masharti ya Serikali.
Nape Nnauye akihojiwa na Kituo cha Television cha ITV alinukuliwa akisema,
“Elon Musk anataka kutoa huduma ya internet hapa, lakini katika mipango yao walikuwa hawana mpango wa kuweka ofisi zao hapa (Tanzania), ikitokea fault (tatizo) mnataka hao wateja wenu waje ofisini kwangu?”.

Waziri Nape aliendelea kusema kuwa haoni sababu ya Starlink kutoa huduma Tanzania ilihali Ofisi za Starlink zipo Marekani na hiyo kwake ni usumbufu kwa Watanzania kwa kuwa wateja hawatakuwa na uwezo wa kupiga simu Marekani linapotokea tatizo.

Uwezo wa Kutumika tena: Kama miradi mingine ya SpaceX, setilaiti za Starlink zimeundwa ili ziweze kutumika tena. Roketi za Falcon 9 huchukua setilaiti kadhaa kwenye anga kila mara ya uzinduzi, na setilaiti hizo huzinduliwa kwa makundi. Uwezo wa kutumika tena kwa roketi hupunguza gharama kubwa ya kupeleka na kudumisha setilaiti za Starlink.
Vifaa vya Wateja: Ili kupata huduma ya intaneti ya Starlink, watumiaji hutumia sahani za satelaiti zenye teknolojia ya kuzingatia mawimbi (phased-array satellite dishes). Saizi hizi za watumiaji zimeunganishwa na teknolojia ya hali ya juu ambayo inaweza kujiweka moja kwa moja na kufuatilia setilaiti angani, ikifanya iwe rahisi kwa wateja kuunganisha na mtandao.
MAJIBU YA WAZIRI NAPE HAYAKUWARIDHISHA WANANCHI.
Baada ya majibu hayo ya Waziri Nape Nnauye ya kuwataka Starlink wafungue Ofisi zao Tanzania ndipo wapewe kibali cha huduma yao kiliwaibua wanateknolojia waliohoji juu ya kauli ya Nape juu ya kuwepo kwa Ofisi Tanzania.
Baadhi ya maswali waliyohoju ni pamoja na je, ofisni za Meta (Facebook, Instagram, WhatsApp) zipo Tanzania?, Je, linapotokea tatizo wateja hawa wanasuluhishaje?
Je, Kampuni ya Google (YouTube, Gmail, AdSense) na huduma nyingine za Google, wana Ofisi zao Tanzania?, Na Je, watumiaji hawa wanapopata tatizo wanawafikiaje Google kutatuliwa matatizo yao?
Maswali yalikuwa mengi ya huduma zitolewazo nchini na makampuni malubwa yakiwemo ya simu na hawana Ofisi Tanzania na linapojitokeza tatizo hutatuliwa.
Wananchi walimkumbusha Waziri Nape Nnauye kuwa akiwa kama Waziri wa Masuala ya Teknolojia hakupaswa kuzungumzia Ofisi (Majengo) kwa kuwa ulimwengu wa sasa kila kitu hufanyika kimtandao na kurahisisha kila jambo kwa wakati kuliko kutumia muda wa kwenda Ofisini.
Waliendelea kusema kuwa, kama Starlink watajenga Ofisi Dar Es Salaam, je mteja wa Mwanza au Bukoba na sehemu iliyo mbali atasafiri kuifuata huduma wakati anaweza kusaidiwa online?
Ufikiaji wa Kimataifa: Lengo kuu la Starlink ni kutoa ufikiaji wa intaneti kwa maeneo yote ya dunia. Kwa kuweka maelfu ya setilaiti katika anga ya chini ya Dunia, mtandao huu utatoa huduma ya intaneti kwa maeneo ambapo miundombinu ya intaneti ya kawaida ni vigumu au gharama ni kubwa sana.
Majaribio ya Beta na Upanuzi: Starlink ilianza kutoa huduma ya majaribio, inayojulikana kama “Better Than Nothing Beta,” kwa watumiaji waliochaguliwa mwishoni mwa 2020.
Wakati wa awamu hii ya majaribio, watumiaji walitoa maoni kuhusu huduma ili kusaidia kuboresha utendaji na uwezo wake. Kadi hii ya setilaiti inaendelea kupanua na setilaiti zaidi zinazozinduliwa, chanjo na ubora wa huduma unatarajiwa kuboresha.